𝗠𝗨𝗗𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗘𝗡𝗚𝗘𝗡𝗘𝗭𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗨𝗧𝗘𝗡𝗚𝗘𝗡𝗘𝗭𝗔
KAMANDA MMOJA ALIWAHI KUNIAMBIA MAMBO MAWILI AMBAYO HUWAAMBIA WAFANYAKAZI WENZAKE, MAMBO HAYA, YALINIKAA SANA NA NIKAYAELEWA Alisema .... *1.* Kila siku kabla ya kulala, andaa sare yako na itundike Karibu na kitanda chako, Unapopanda kitandani, iangalie sare yako na kisha jiulize.... kitatokea nini nisipovaa sare hii na nikajaribu kuingia kwenye maeneo ya jeshi? Jibu lake ni, hakuna saluti yeyote itakuja njia yako! Kwanza utasimamishwa getini na kuulizwa maswali! Na ikitokea mwingine amevaa sare hii hii na akapita pembeni ya mlinzi wa jeshi, hakika atapewa saluti. Hivyo basi, saluti haikuwa ya kwako bali ni ya sare iliyotundikwa ukutani ambayo imekutengeneza lakini kumbuka, sare hiyo haitakuwa ya kwako milele! Siku moja itaenda kwa mwingine.... Kwahiyo, jiandae kwa hilo tafadhali! *2.* Kila siku ukimaliza kazi zako, hakikisha kila mtu ametoka ofisini kwako. Nyanyuka kwenye kiti chako, tembea elekea upande ule mwingine, kaa kwenye kiti, na kisha kitazame kiti chako. Huenda kw...