MAFANIKIO YAKO YA MAARIFA NI TIJA KWA MAISHA YAKO HAPO BAADAE🔥

👊 📡 MAFANIKIO📡


Mfumo wa maisha katika baadhi ya familia za kitanzania ni ule ule ulio kuwepo tangu miaka ya mababu zetu.


Baadhi ya familia zimeweza kuhama katika mfumo wa maisha ambao ulikuwepo huko nyuma lakini baadhi ya familia zime shidwa kabisa . 


Swala la baadhi ya familia kushindwa kuhama kutoka kwenye mfumo wa maisha  ambao ulikuweka tangu enzi ndio unao endelea kutoa matokeo kwa vijana kuanza kumiliki pesa nyingi / kuwa tayari akiwa na umri mkubwa .


Baadhi ya vijana wengi ambao wanatokea katika familia ambazo hazija hama kutoka katika mfumo wa maisha amabo ulikuwepo tangu enzi wengi huwa wanaanza kupata muda wa kufurahia mafanikio yao ya kimaisha wakati wakisha kuwa na umri wa uzee . 


Lakini kwa vijana ambao wametoka kwenye familia ambazo ziliweza kuhama kutoka kwenye huo mfumo basi wameweza kuanza kumiliki na kufurahia mafanikio yao yakimaisha wakiwa na umri mdogo.


Kwa kawaida kijana anapo kuwa na umri wa miaka 20 anatakiwa awe na umiliki wa pesa kuanzia Tsh : 5,000,000 pamoja na kuwa na umiliki wa biashara au kampuni. 


Lakini cha ajabu kijana hadi anamaliza chuo kikuu , hana hata biashara, hana kampuni wala Bank Account yake haina Ths : 5,000,000 . Kwa hili ni razima baadhi ya jamii endelee kulalamika kuhusu ugumu wa maisha .


Kukibwa ugumu wa maisha tuna utengeneza sisi wenyewe .


📡Ramakhan-0fficial📡

Comments

Post a Comment

Popular Posts